Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Antiphas Lissu amefunguka kwamba atarudi nchini siku atakayopona kwani
Ulaya siyo kwao na kwa umri alionao hataweza kujifunza namna ya kuishi katika
nchi za huko.
Lissu ameyasema hayo kupitia video
fupi iliyorekodiwa na Mtanzaia Damian aishiye Uholanzi ambaye alikwenda kumuona
katika hospitali aliyolazwa huko nchini Ubelgiji.
Lissu ameeleza kuwa kwa sasa anachosubiri
ni kufanyiwa oparesheni moja itakayofanywa mwezi ujao na baadae ataanza
matibabu ya kufanya mazoezi ya viungo na baada ya matibabu hayo yote
wataweza kurejea nchini.
Lissu amesema kuwa ni lazima atarudi
nchini Tanzania kwa kuwa umri alionao kwa sasa siyo umri wa kuanza kujifunza
namna ya kuishi katika nchi hizo za ulaya ikiwa ni pamoja na kuhangaika
kutafuta kazi.
Mbali na hayo Mbunge huyo ametoa
ahadi kwa watanzania kuwa hatakuwa na cha kuwalipa pindi atakaporudi Tanzania
bali atajitahidi kwa kadri yoyote ili kuhakikisha anatoa uwakilishi unastahili
watanzania.
Lissu amesema kuwa baada ya serikali
pamoja na Bunge kumtelekeza watanzania kwa umoja wao walihakikisha wanapambana
kumuombea ikiwa ni pamoja na kutoa michango mbalimbali iliyomuwezesha yeye
kupatiwa matibabu tangu akiwa hajitambui mpaka hatua ya sasa aliyofikia ambayo
amebakiza oparesheni moja tu kwa mujibu wa Madaktari.
"Mbali na kuwa watanzania
waliniombea sana lakini pia walinilea. Sijui kama kuna bei ambayo ninaweza
kuwalipa wananchi wa Tanzania kwa upendo walionionyesha pamoja na kunitibu.
nawashukuru kwa upendo wao. Nawaahidi kulipa hilo deni kwa kutoa uwakilishi
unaostahili ukarimu wao," Lissu.
Lissu atoa kauli ya kurudi Tanzania
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment