Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi ISACK KAMWELWE
amesema serikali haitamvumilia mtendaji wa serikali na mtu yeyote atakaye
kwamisha na kuhujumu juhudi za serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata maji
safi na salama kwa kuwa baadhi ya watumishi inadaiwa wamekuwa wakipokea rushwa
na kufifisha juhudi hizo
Mhandisi KAMWELWE ametoa kauli hiyo alipokuwa akizundua bodi
mpya ya Mamlaka ya Maji Jiji la Arusha, baada ya kuivunja bodi ya awali kwa
madai ya kushindwa kutekeleza ipasavyo majukumu yake
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bwana MRISHO GAMBO amesema maji ni
moja ya tatizo kubwa kwa Mkoa wa Arusha na serikali imewekeza fedha nyingi
kuondoa tatizo hilo hivyo hawatavumilia aina yoyote ya ufujaji wa miradi ya
maji inayotekelezwa
Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Mhandisi RICHARD MASIKA
amesema bodi yake itafanyakazi kwa weledi wa hali ya juu na hakuna kitakacho
kwenda kinyume na matarajio
Atakaye hujumu juhudi za Serikali wananchi wakose maji kukiona.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment