Utafiti uliofanywa na Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI
TACAIDS umeonyesha asilimia 40 tu ya wanaume wanaogundulika kuugua
maradhi hayo ndio wanafanya vipimo na kutumia dawa za kufubaza makali ya
ugonjwa huo hali inayochangia idadi ya vifo kuongezeka katika kundi hilo
Takwimu hizo zinatolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TACAIDS Jumanne Isango katika mkutano wa kuzijengea uwezo konga za waishio na
virusi vya ukimwi kuhusu sheria ya ukimwi ambapo anasema tafiti
zinaonyesha wanaume wanaongoza kwa idadi ya vifo kutokana na kuchelea
kutumia dawa za kufubaza makali ya ugonjwa huo
Kwa upande wake Mkurugenzi wa ufuatiliaji na tathmini kutoka
TACAIDS Dk Jerome Kamwela anasema asilimia 52 tu ya Watanzania wanaoishi na
virusi vya ukimwi ndio wanajua hali zao ambapo kati yao asilimia 90 wanatumia
dawa za kufubaza virusi
Cosmas Kurwa ni Hakimu kutoka Dodoma anahoji kuhusu matumizi
ya misaada inayotolewa na mataifa wahisani katika vita ya ungonjwa huo kuwa
vina masharti kwenye matumizi yake huku Rose Kosuri ambaye ni muathirika wa
maradhi hayo akitaka kujua uhalali wa taarifa za watu wanaofanya vipimo binafsi
vya ugonjwa huo
Asilimia 40 ya wanaume wenye UKIMWI ndo hutumia dawa za kufubaza
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment