Nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu amesema, hana bifu
na Hamisa Mobetto, ila pia si rafiki yake.
Wasichana hao walikuwa marafiki lakini hivi karibuni
zilienea taarifa kuwa wamegombana.
Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006 amesema hana tatizo na
msichana huyo ila alimchukia baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa akimuongelea
vibaya kwa watu.
"Sina bifu na Hamisa ila siyo rafiki yangu kabisa
kuna maneno aliniongelea mabaya… tena sio kwa kuhadithiwa, nilimsikia akiwa
amerekodiwa… sasa nikaona huo ni unafiki kwa hiyo nikaona kila mtu achukue muda
wake,"amesema Wema.
Amesema, akikutana na Hamisa hataki salamu na
mwanamitindo huyo, kila mtu afanye mambo yake.
Hamisa amezaa na Naseeb Abdul ‘Diamond’ na hivi karibuni
mwanamuziki huyo alitupia video ya wawili hao wakiwa kwenye mikao ya kimahaba.
Wema na Diamond walikuwa wapenzi, waliachana na
kurudiana takribani mara mbili kabla ya kuachana tena kwa ugomvi mpaka kufikia
hatua ya kutosalimiana.
Takriban miezi miwili iliyopita, Wema na Diamond
walionekana pamoja na wenyewe wanadai wamekuwa marafiki wa kawaida si wapenzi
tena.
Wema Sepetu: - Sitaki salamu ya Hamisa Mobeto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment