Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amemuwakilisha Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa
Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC aliyemaliza muda wake
kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili wa SADC kuhusu hali
ya Usalama katika Kanda umefanyika hapa Luanda, leo tarehe 24 Aprili, 2018.
Mkutano huu umeitishwa baada ya
mashauriano kati ya Mheshimiwa Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika
Kusini na Mwenyekiti wa SADC na Mhe. João Lourenço, Rais wa Angola na
Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikino ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC
Mkutano huu umetanguliwa na kikao
cha Mawaziri ambacho kilifanyika jana tarehe 23 April 2018.
Mkutano huu ulihusisha nchi
wanachama sita tu wa SADC Double Troika na Viongozi wafuatao walihudhuria,
Mhe. Dkt. Cyril Ramaphosa, Rais wa
Afrika Kusini na Mwenyekiti wa Summit, Mhe. João Lourenço , Rais wa
Angola na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na
Usalama – (SADC Organ on Politics, Defence and Security Cooperation),Mhe. Hage
Geingob, Rais wa Namibia na Makamu Mwenyekiti wa Summit, Mhe. Edgar Lungu, Rais
wa Zambia na Makamu Mwenyekiti wa SADC Organ, Mfalme Mswati III, Mfalme wa
Swaziland na Mwenyekiti wa Summit anayetoka;
Mheshimiwa Joseph Kabila Kabange,
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mheshimiwa Thomas Thabane, Waziri
Mkuu wa Lesotho walialikwa na walihudhuria.
Mkutano huu utapitia na kujadili
ajenda zifuatazo:-
1. Hali ya siasa na usalama katika Falme ya Lesotho;
2. Hali ya siasa ulinzi na usalama katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo;
3. Hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Madagascar; na
4. Masuala ya demokrasia katika kanda ( Consolidation of
Democracy in the region)
KUHUSU HALI YA SIASA, ULINZI NA
USALAMA NCHINI LESOHO:-
1. Mkutano huu umevitaka Vyama vyote vya Siasa kulipa
uzito suala la Mjadala wa Kisiasa na Mchakato wa Mageuzi ya Kisekta na
kushiriki kikamilifu kwenye michakato yote ili kupata suluhisho la kudumu
katika changamoto za kiusalama na kisiasa;
2. Pia Mkutano huu umeitaka Serikali ya Lesotho na wadau
wengine kukamilisha mjadala wa kitaifa ifikapo mwezi Juni, 2018 na kutoa
taarifa kwenye kikao kijacho cha kawaida cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC
ambacho kimepangwa kufanyika Augosti, 2018;
3. Pia Misheni ya Ulinzi nchini Lesotho (SADC Preventive
Mission in the Kingdom of Lesotho – SAPMIL ) imeongezewa muda kwa kipindi
kingine cha miezi sita kuanzia Mei 20, 2018.
KUHUSU HALI YA SIASA,
ULINZI NA USALAMA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
(DRC)
Nchi wanachama zitaombwa kuisaidia
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwenye kipindi
hiki wanachoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu kwa lengo la kuhakikisha kuwa uchaguzi
huu unafanyika katika mazingira ya amani.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano
huu ulitumia fursa hiyo kuomba nchi wanachama wa SADC kumuunga mkono Mheshimiwa
Stephen Maselle ( Mb), ambaye anawania nafasi ya Makamu wa Rais wa Bunge
la Afrika ( Deputy President of the Pan African Parliament).
Makamu Wa Rais Amuwkilisha Rais Magufuli Kwenye Mkutano Wa SADC Double Troika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment