Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA kimelitaka Jeshi la Polisi nchini kutoa taarifa rasmi juu ya matukio ya
kuwakamata na kuwapekua viongozi wa kisiasa katika ngazi mbalimbali nyakati za
usiku bila ya kuwepo na sababu zozote zenye misingi ya kisheria.
Hayo yameelezwa na taarifa
iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini
Makene leo Aprili 25, 2018 na kusema jeshi hilo limeendelea kuwashikilia
kinyume cha sheria kwa kuwanyima dhamana na kutowafikisha mahakamani
Aidha, Makene amesema baadhi
ya maeneo ambayo hadi sasa viongozi wa CHADEMA wamekumbana na manyanyaso na
ukiukwaji huo mkubwa wa haki za binadamu na sheria za nchi unaofanywa na polisi
ni Dar es Salaam, Geita, Pwani, Njombe, Iringa, Arusha, Morogoro na Tanga.
"Tunapinga na kulaani vikali
vitendo hivyo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria za nchi yetu na
tunasisitiza kuwa havikubaliki katika jamii yeyote inayozingatia kuwa haki ni
msingi muhimu wa amani na utulivu wa kweli.Tunatumia nafasi hii kulikumbusha
Jeshi la Polisi nchini kuwa lina wajibu wa kutekeleza majukumu yake kwa
kuzingatia Katiba, Sheria za Nchi na weledi unaokubalika", amesema Makene.
Kwa upande mwingine, Makene amesema
chama chake kimetoa maagizo kwa wanasheria wake kupitia Kurugenzi ya Katiba na
Sheria, kufuatilia suala hilo kwa ukaribu na kuchukua hatua za haraka za
kisheria.
CHADEMA yatoa tamko
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment