Waziri mkuu atembelea mradi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kwamba ameridhishwa na maendeleo yake.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika Juni 2019 na utakuwa na uwezo wa kuegesha Ndege kubwa 24 kwa wakati mmoja, pamoja na kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Ijumaa, Machi 23, 2018) amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo pamoja na kukuta Watanzania wengi wakishiriki katika kazi za ujenzi.
Waziri mkuu atembelea mradi Waziri mkuu atembelea mradi Reviewed by KUSAGANEWS on March 24, 2018 Rating: 5

No comments: