Jeshi la polisi Morogoro
limewakamata watu wawili ambao wanadaiwa kuwa ni watekaji wa watu na
kujihusisha na matukio ya ubakaji kisha kuwapiga picha za utupu waliowafanyia
vitendo hivyo kwa lengo la kuwatisha kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa watu
hao wawili na kusema kuwa wapo watu wengine watatu pia wamekamatwa kwa kufanya
wizi kupitia njia ya mitandao ya kijamii.
"Ni kweli tumemkamata mtuhumiwa
mmoja akiwa na mwenzake wanaojihusisha na utekaji wa watu, kuwabaka kisha
kuwapiga picha za utupu na kuwatishia kuzisambaza picha hizo kwenye mitandao ya
kijamii kama hawata toa fedha lakini mbali na hao wawili tunawashikilia watu
wengine watatu ambao wao wamekuwa wakifanya wizi na utapeli kwa njia za
mitandao ya kijamii" alisema
Kamanda Matei
Aidha Kamanda Matei amesema kuwa
uchunguzi utakapokamilika watu hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao
kutokana na makosa hayo.
Watekaji na wabakaji wakamatwa Morogoro
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 26, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment