Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
anayeshughulikia ajira, Jenista Mhagama jana aliwakabidhi wanawake 600 wakazi
wa Arusha, hundi ya Sh120 milioni ikiwa ni mkopo usio na riba
Fedha hizo zimetolewa na ofisi ya mkuu wa
Mkoa wa Arusha akisaidiana na jumuiya ya wafanyabiashara Arusha, katika mkakati
wa kusaidia makundi maalumu wakiwamo walemavu na wanawake
Katika fedha hizo kila mwanamke atapokea
mkopo wa Sh200,000
“Naamini utawasaidia mliokopeshwa mtarejesha
kwa wakati,” alisema Mhagama
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi na
Ajira), Anthony Mavunde alisema “Fedha ya leo iwe mbegu inayokwenda kubadilisha
maisha ya kina mama hawa kwani kila jambo linawezekana nakupongeza (Mrisho)
Gambo kwa kuwawezesha wanawake hawa,” alisema
Gambo ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Arusha
alisema mkopo huo unatolewa bila kujali itikadi ya vyama na wanaokopeshwa
wamepatikana kutokana na utaratibu uliofanywa katika ofisi za mitaa na kata 25
za jiji la Arusha
Kuhusu kina mama hao waliokopeshwa, mkuu wa
Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro aliwaelezea kuwa ni kama hewa ya oksijeni
kwani wanahakikisha mahitaji yote ya familia yanapatikana ikiwamo kubuni
biashara za kujikwamua kiuchumi.
Wanawake 600 wakopeshwa Sh120 milioni bila riba Arusha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment