Simanjiro. Wananchi wa Kijiji cha
Langai, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wamemgomea Mkuu wa wilaya hiyo,
Zephania Chaula kugawa ardhi yao wanayodai kuimiliki kihalali.
Wakizungumza katika mkutano wa
hadhara, wananchi hao wanaojishughulisha na kilimo na
ufugaji wamesema hatua hiyo ya mkuu wa wilaya ni ubaguzi.
Mmoja wa wananchi hao, Paulo
Simtek amesema wafugaji wamekuwa wakiishi eneo hilo kwa muda mrefu,
lakini kitendo cha mkuu wa wilaya kuchukua mashamba yao, kuyamega na
kuwapatia wakulima kunaweza kuibua migogoro.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Langai,
Mathayo Ole Silongoi amesema kuwa sintofahamu hiyo inatokana na
wa uongozi wa wilaya kudharau Serikali ya kijiji na kufanya uamuzi
usiowahusu kwani mashamba hayo yako chini ya Serikali ya kijiji.
Akizungumzia suala hilo, Chaula
amesema uongozi wa kijiji hicho umekuwa na ubaguzi wa jamii na ndicho
chanzo cha migogoro na kwamba, Serikali itachukua hatua za
kisheria dhidi yao ikiwemo kutoitisha mikutano ya kijiji tangu
walipochaguliwa
"Huo uongozi wa kijiji hatua
za kisheria zinawafuata kwa kukiuka ya uongozi wao waache kusema
nimegawa ardhi, bali waseme wao wamefanya nini ikiwemo kuitisha mikutano
kusikiliza kero za wananchi na kusoma mapato na matumizi zaidi wanayoyafanya
ni kuendekeza ubaguzi wa ukabila," amesema Chaula
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Simanjiro, Jakson Siptek amesema wameanza kuchukua hatua za utatuzi
na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati hatua zinaendelea.
|
|
WANANCHI WADAI MKUU WA WILAYA KUFANYA UBAGUZI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment