Wafanyabiashara na wawekezaji
nchini wameeleza kero na changamoto wanazokutana nazo katika uendeshaji wa
shughuli zao, huku wakibainisha kuwa zimekuwa zikirudisha nyuma dhamira ya
Serikali katika kukuza sekta binafsi nchini.
Wametoa kauli hizo leo Jumatatu
Machi 19, 2018 Ikulu Dar es Salaam katika mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la
Biashara, huku hoja zao zikichukuliwa na mwenyekiti wa baraza hilo, Rais John
Magufuli.
Kabla ya kuanza majadiliano hayo,
Rais Magufuli amesema leo utafanyika mjadala wa kuleta mabadiliko
ambapo kila mfanyabiashara atasimama na kueleza kero na changamoto
zinazomkabili, zitapatiwa majibu na watendaji wa Serikali, wakiwemo mawaziri
“Leo kuna watu kama 13 kutoka Tume
ya Mipango, nataka tuzungumze leo kwa uwazi, mimi hata tungezungumza leo na
kesho sawa tu tuendelee , nataka mseme kwa uwazi, dakika tatu kila mmoja
atazungumza , nataka tu-solve problem sio kila mara tunakutana hapa
tunajadili mambo yaleyale,”amesema Rais Magufuli
Mfanyabiashara Mwita Gachuma
kutoka Mwanza ndiye ameanza kufungua mjadala huo akitoa kero mbili ikiwamo
tozo kubwa zinazotozwa nchini ikilinganishwa na nchi jirani kama Kenya
“Kwa nchi za jirani wanatoza
kuanzia asilimia 11, 13, sisi (Tanzania) tunatozwa asilimia 33, asilimia 15
tunatakiwa kurudishiwa lakini hata hivyo haturudishiwi hiyo asilimia 15,
hatua hiyo inaathiri hata mzunguko wetu wa fedha,”amesema.
Mfanyabiashara mwingine kutoka Geita
aliyejitambulisha kwa jina moja la Sospeter amezungumzia pia kero ya
kodi katika usafirishaji wa bidhaa.
Amesema TRA imekuwa ikikadiria
kodi kubwa tofauti na kiwango cha mzigo
“Kwa mfano gunia la kilo 100
unaambiwa ni zaidi ya kilo 100. Kwa hivyo inaathiri sana na matokeo yake
unajikuta mfanyabiashara unabeba mzigo kidogo, kwa hiyo tunaomba ulitazame
hilo,”amesema
|
|
WAFANYABIASHARA WAFUNGUKA MBELE YA RAISI MAGUFULI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 19, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment