Akizungumzia Madhumuni ya kutoa elimu hiyo Kaimu meneja wa Mamlaka ya mawasiliano kanda ya Kaskazini Francis Msungu amesema ni katika jitihadha zilezile za serikali za kuhakikisha kwamba inamlinda mlaji kwa kumpa elimu juu ya haki na wajibu wawatumiaji wa huduma za mawasiliano kwaajili ya kuleta maendeleo.
Katika kuadhimisha siku ya walaji wameitumia kutoa elimu juu ya haki, na wajibu wa watumiaji wa huduma za mawasiliano kama sehemu ya walaji,tahadhari za kuchukua katika mawasiliano hususani mitandao.
Msungu amesema kwamba walaji,ni kundi kubwa la kiuchumi ambalo huwa linaadhirika na kuathiri maamuzi ya kiuchumi yanayofanywa na mataifa na makampuni ya kibiashara.
"Sisi kundi hili la walaji ni kundi lile ambalo maoni yetu huwa usual a to kusikilizwa kwa makini katika maamuzi ambayo yanafanywa ya kiuchumi" alisema.
Kwa upande wake Mhandisi Mwandamizi wa Masafa (TCRA) Jan Kaaya ametoa tahadhari kwa jamii kutokuweka taatifa nyingi zinazowahusu kwenye mitandao kwani siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la uhalifu ambalo wanatumia mitandao kufuatilia taarifa za watu.
TCRA:: Epukeni Kuweka Taarifa Nyingi Zinazowahusu Kwenye Mitandao Ya Kijamii
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment