Mchungaji wa KKKT usharika wa Karanga Moshi Akamatwa Kwa kinachodaiwa kuwa ni uchochezi

MOSHI, KILIMANJARO: Mchungaji Fredy Njama wa Usharika wa Karanga, KKKT Dayosisi ya Kaskazini, amekamatwa na Polisi kwa kinachoidaiwa kuwa ni “Uchochezi wa kisiasa”.

Mchungaji huyo wiki mbili zilizopita alisoma ripoti katika mkutano mkuu wa mwaka wa usharika wake ambayo ndo imepelekea kukamatwa kwake.

Katika ripoti hiyo, alibainisha kuwa mapato ya usharika yanapungua kwa sababu mbalimbali
-
Katika utangulizi wa ripoti alitaja changamoto 6 zinazoikabili nchi kwa sasa: Ukosefu wa ajira kwa vijana, Hali ya uchumi inayoyumba, Hali ya kisiasa ni ya mashaka, Gharama kubwa za matibabu, Sera ya elimu bure na Wastaafu kutolipwa mafao yao

Ripoti hiyo pia imechapwa ktk kijitabu na kiwanda cha uchapaji cha Dayosisi hiyo

Kundi la Polisi na maafisa usalama walimchukua Ijumaa asubuhi hadi kiwandani na kumtaka akusanye vijitabu vyote hadi vilivyosambazwa na kuvikabidhi Polisi. Aidha walimtaka aandike barua kuomba radhi na kufuta ripoti hiyo
-
Jioni  jana, Polisi walifika ofisi ya usharika na kufanya upekuzi. Walichukua laptop na flash. Kisha walimpakia mchungaji katika gari lao na kuondoka naye.
Mchungaji wa KKKT usharika wa Karanga Moshi Akamatwa Kwa kinachodaiwa kuwa ni uchochezi Mchungaji wa  KKKT usharika wa Karanga  Moshi  Akamatwa Kwa kinachodaiwa kuwa ni uchochezi Reviewed by KUSAGANEWS on March 17, 2018 Rating: 5

No comments: