Serikali ya Uganda
imesaini makubaliano na nchi jirani ya Kenya ya kuiuzia tani laki sita za
mahindi kila mwaka, hatua ambayo inatoa uhakika wa soko kwa wakulima wa mahindi
wa Uganda ambao kwa miaka mingi wamehangaika kuuza mahindi ya ziada.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza
la Nafaka la Uganda, Chris Kaijuka, bado shehena kubwa ya mahindi inasafirishwa
kwenda katika nchi mbalimbali bila kibali maalum ikiwemo Rwanda, Sudan na
Kenya.
Imebainika kuwa Uganda huzalisha
takriban tani milioni nne za mahindi kwa mwaka, ambapo kiasi kidogo sana
hutumika nchini humo huku 80% yakisafirishwa kama nafaka kwenda kwenye masoko
ya Kikanda.
Mmoja wa wasafirishaji wa mahindi
kutoka Uganda, Haji Abudalla Kamira, amesema chini ya makubaliano hayo sasa
tani moja ya mahindi itauzwa kwa dola za Kimarekani 225 katika soko la Kenya
Raisi wa Uganda na Kenya Wasaini mkataba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment