Mwanamuziki wa Bongo fleva na CEO wa label ya WCB, Diamond
Platnumz amefunguka na kusema kuwa chombo chochote cha habari ambacho
kinaibania WCB kwa njia yoyote basi kitapotea kwani yeye ni kama maji
usipokunywa utayaoga.
Diamond amekuwa mmoja wa wasanii ambaye amekuwa na migogoro na
media mbali mbali ambapo siku za hivi karibuni Kumekuwa na sintofahamu kati
yake na mkurugenzi wa Clouds Fm, Ruge Mutahaba.
Hii imekuja baada ya Diamond kutangaza kuanzisha stesheni zake
za redio na Tv ambazo ni Wasafi Radio na Tv ambavyo amesisitiza vitacheza
nafasi kubwa katika kukuza mziki wake na hata wasanii kutoka WCB kwa ujumla.
Diamond hivi sasa yuko nchini Kenya, Nairobi ambako ameenda
kwenye uzinduzi wa albamu yake ya ‘A boy from Tandale’ ambayo inategemewa
kuanza kuuzwa hivi karibuni.
Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Diamond amefunguka kuhusu
albamu yake ambayo ndani yake kuna nyimbo ambazo amewashirikisha wasanii kadhaa
ikiwemo Rick Ross, Neyo na Omarion.
Lakini pia Diamond amefunguka kuhusu Wasafi Tv na Redio ambavyo
vinategemea kuanza kuruka hewani siku za hivi karibuni lakini Diamond
ameshangaa media zinazotaka kubania mziki wake kwani yeye ndio burudani yenyewe
kwaiyo wao kumzuia yeye wanapotea:
"Yaani mimi nimejiwekea mazingira ambayo hata nikilala
chumbani lazima utaniongelea huwezi kulala bila kunitaja aidha utawataja watoto
wangu, au wasanii wa WCB au hata wapenzi wangu yaani Diamond ni kama Azam vile
au mimi kama maji aidha utaninywa au utanioga yaani utajua mwenyewe lakini mimi
huwezi kulala bila kunitaja kwaiyo media zinazozuia kazi zangu wanapoteza muda
maana mimi ndio burudani na mzalisha burudani”.
DIAMOND AVITISHA VYOMBO VYA HABARI VISIVYOCHEZA NYIMBO ZA WCB
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment