Rais Magufuli amefanya
uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC), Mkurugenzi wa
Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Benjamin Mkapa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi amethibitisha hilo na kusema kuwa Rais Magufuli amemteua Prof. Lazaro
S.P. Busagala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) kuanzia
tarehe 22 Machi, 2018.Kabla ya uteuzi huo Prof. Busagala alikuwa Makamu Mkuu wa
Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) – Taaluma na Utafiti.
Lakini pia Mhe. Rais Magufuli
amemteua Prof. Damian Gabagambi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la
Taifa (NDC) kuanzia tarehe 22 Machi, 2018. Prof. Gabagambi anachukua nafasi ya
Bw. Mlingi Elisha Mkucha ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo
Prof. Gabagambi alikuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kilimo – Sokoine
(SUA).
Aidha Rais Magufuli amemteua Dkt.
Deodatus Michael Mutasiwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya
Benjamin Mkapa Dodoma, Dkt. Alphone Bilola Chandika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Rais Magufuli ateua watatu na kutumbua mmoja
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment