Arusha. Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Adili iliyopo katika jiji la Arusha,Joel Mbaga(27) jana amefikishwa mahakamani ya wilaya yaArusha,kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wa kiume wa miaka 13.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali,Naomi Mollel akitoa maelezo ya kesi hiyo mbele ya hakimu mkazi mahakama wilaya Arusha, Patricia Kisinda alisema, Mwalimu alitenda kosa hilo kati ya mwezi septemba na Octobar mwaka jana.
Akitoa ushahidi katika kesi hiyo jana shahidi wa kwanza,Mama wa mtoto huyo,Agness John(41) alisema, alibaini mwalimu huyo kutenda unyama huo baada ya mtoto wake aliyekuwa kidato cha kwanza katika shule hiyo ya Bweni kugoma kwenda shule.
"Ilikuwa October 30 mwaka Jana, mtoto alirudi nyumbani na kugoma kwenda shule na baada ya kumuhoji alisema mwalimu alikuwa akimlawiti" alisema
Alisema baada ya kumchunguza alimkuta na michubuko sehemu za siri na ndipo alikwenda kutoa taarifa polisi na alimpeleka hospitali ya mkoa ya mount Meru
Agness alisema , baada ya kumfikisha hospitali mtoto wake huyo,alilazwa siku mbili na alibainika kuingiliwa sehemu za siri
Hata hivyo,Mwalimu Mbaga alikana tuhuma hizo .
Hakimu Kisinda iliahirisha kesi hiyo hadi April 3 mwaka huu, ambapo shahidi wa tatu ambaye ni Daktari aliyomchunguza mwanafunzi huyo atatoa ushahidi na mwalimu huyo ataendelea kuwa nje kwa dhamana.
Mwisho

Mwalimu kizimbani kwa kimlawiti mwanafunzi.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 12, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment