Akifungua kikao kazi cha 14 cha maafisa habari, mawasiliano na mahusiano, mkoani Arusha Jana Dk. Mwakyembe alitoa maagizo kwa maafisa hao kuwa baada ya mkutano huo unaotarajiwa kudumu kwa siku tano kumalizika ni wajibu wa kila mshiriki kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ambapo alisema watakaokiuka hatua za kisheria zitafuata.
Alisema kuwa wapo maafisa habari wazembe wasiojishughulisha na kutafuta habari za wizara, taasisi na kusubiri hadi taasisi itangaze kuwepo kwa mkutano, ziara na mambo kama hayo jambo alilosema ni uzembe na kudhalilisha taaluma huku akiwataka kwenda na wakati kutoa habari za taasisi,Halmashauri kila Mara ili kuhabarisha umma na serikali kwa ujumla.
"Kama kuna maafisa habari wanaokaa ofisini kusubiri hadi itokee mkutano au ziara bila wao kutafuta habari za wizara husika basi ni tatizo na tutawahesabu kama maafisa habari hewa" alisema mwakyembe.
Aliwataka pia kujenga ushirikiano mzuri baina yao na vyombo vya habari v ilivyo wazunguka ili kuhakikisha taarifa zinafikia umma ambapo alisema siyo kila taarifa ni taarifa ya kutoa bali zile zilizosahihi ambapo ushirikiano kati ya vyombo vya habari na Maafisa hao utafanya kufikisha taarifa sahihi.
Alizitaka wizara, Halmashauri, pamoja na taasisi kuwapatia vifaa vya kazi maafisa habari ili waweze kutekeleza majukumu kwa urahisi ambapo alisema kama wizara au taasisi haziwapatii vifaa hiyo ni changamoto na taasisi, wizara hizo zitakuwa tatizo.
Aliongeza kuwa Halmashauri ambazo hazina maafisa habari hazitavumilika kwa kipindi cha utawala huu kwa kuwa kila jambo linatakiwa kufanyika kimkakati ili kufikia uchumi wa viwanda.
Naye mwenyekiti wa chama cha maafis mawasiliano serikalini (TAGCO) Pascal Shelutete alisema lengo la kuanzishwa kwa Chama hicho ni pamoja na kuhakikisha inaendeleza tasnia ya mawasiliano katika weledi unaotakiwa kwa wanatasnia wote kutoka serikali kuu hadi serikali za mitaa.
Kwa upande wa mwakilishi wa Umoja wa mataifa Alvaro Rodriguez alisema Umoja wa mataifa unapenda kuwa washirika wa serikali katika mawasiliano ya maendeleo nchini kwa kuwa nao ni watumishi wa umma.
Hata hivyo kauli mbiu ya mkutano huo wa maafisa habari,mawasiliano,Mahusiano na itifaki ni ' Je Mawasiliano ya kimkakati yanachangiza vipi Tanzania ya viwanda'
Mwishooo.
Mwakyembe awaonya maafisa habari
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 12, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment