Mwalimu ashikiliwa na polisi kwa kumkashifu Raisi Magufuli


Mwalimu wa shule ya sekondari ya Nyakisasa iliyopo mkoani Kagera aliyetambulika kwa majina ya Deogratias Simon anashikiliwa na jeshi la polisi Kagera kwa tuhuma za kumkashfu Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Mwalimu huyo anadaiwa kutenda kosa hilo mwaka 2016 kupitia mitandao ya kijamii ambapo inadaiwa alikuwa akisambaza ujumbe ambao polisi wanaona ulikuwa na lengo la kumchafua Rais Magufuli. 

Jeshi la polisi Kagera litamfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo baada ya uchunguzi kukamilika ili kumshtaki kwa kosa hilo analodaiwa kulifanya mwaka 2016.

Mwalimu ashikiliwa na polisi kwa kumkashifu Raisi Magufuli Mwalimu ashikiliwa na polisi  kwa kumkashifu Raisi  Magufuli Reviewed by KUSAGANEWS on March 22, 2018 Rating: 5

No comments: