Mfuasi wa CHADEMA,
Ally Rajabu anayekabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali ameieleza
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anaomba arejeshewe gari lake ambalo lipo
mikononi mwa polisi.
Ally Rajabu ni
mshtakiwa wa 28 kati ya 31 wakiwemo watatu waliopigwa risasi na Polisi ambao ni
wafuasi wa chama hicho wanaokabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali
maeneo ya Kinondoni Mkwajuni Dar es Salaam.
Awali kabla ya kueleza
hayo, Wakili wa Serikali Aldo Mkini, amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard
Mashauri kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.
Naye Wakili wa
utetezi, Alex Massaba amedai kuwa wateja wake wawili ni wagonjwa na wameshindwa
kufika mahakamani hapo.
Baada ya kueleza hayo,
mshtakiwa wa 28, Ally Rajabu ameieleza mahakama kuwa anaomba kurudishiwa gari
lake ambalo linashikiriwa na Jeshi la Polisi tangu siku ya maandamano.
Hata hivyo, Hakimu
Mashauri amesema kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kuingilia masuala
yaliyofanyika Polisi ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi April 4, 2018.
Washtakiwa wengine
katika kesi hiyo ni Thabitha Mkude, Khaji Lukwambe, Emmanuel Kimio, Mohamed
Juma, Husein Mnimbo na wenzao kwa pamoja wanadaiwa kati ya February 16,
2018 maeneo ya Mkwajuni Kinondoni DSM walifanya mkusanyiko usio wa halali
kinyume cha sheria.
Mtuhumiwa wa Maandamano ya CHADEMA awadai polisi gari yake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment