Ama kweli kuishi kwingi kuona mengi: Hivi ndivyo unaweza kusimulia mkasa wa mtoto anayekadiriwa kuwa na miaka mitano alivyomfikisha baba yake mzazi kituo cha polisi huko Ngara mkoani Kagera.
Kisa chenyewe ni baada ya mtoto huyo kudai kubaini njama
za baba yake kutaka kuuza shamba bila kuishirikisha familia yake hali ambayo ilimghadhabisha
mtoto huyo na kwenda kumshitaki.
Picha ya video fupi iliyorekodiwa kwa njia ya simu juu
ya mkasa huo ilizagaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuibua mjadala miongoni
mwa makundi ya WhatsApp, Facebook na Instagram.
Sababu iliyowashtua na kuwavutia watu wengi ni umri wake
unaokadiriwa kuwa miaka mitano na uwezo wake wa kupambanua mambo hadi kuchukua
hatua ya kumshtaki baba yake ili kumzuia asiuze shamba lao.
Mtoto huyo alieleza namna alivyochukizwa na kitendo cha
baba yake kutaka kuuza shamba.
"Anataka kuuza shamba sasa tutaishi wapi?"
Anahoji mtoto huyo na kusema kuwa alimkuta baba yake akiandikishana na mteja na
ndipo alipochukua uamuzi wa kwenda kumshtaki polisi.
Alieleza kuwa alitoka nyumbani kwao kijiji cha Kabanga
wilayani Ng'ara mkoani Kagera hadi Polisi kwa kupanda lifti ya mtu aliyemtaja
kwa jinala Thabiti.
Mtoto huyo ambaye alionekana kujibu maswali aliyokuwa
akiulizwa kwa kujiamini, alisema alipowaeleza kuhusu mkasa huo polisi walirudi
naye hadi nyumbani na kuzuia mauziano hayo.
"Polisi walikuja wakamuuliza baba kama kweli
anataka kuuza shamba, baba akasema
hajauza...wakataka kumpeleka kituoni, nikakataa...," anaeleza zaidi.
Mtoto huyo aliyekuwa akijieleza kutokana na maswali
aliyokuwa akiulizwa njiani, alijieleza zaidi kuwa hana mama na anaishi na baba
yake huyo peke yao.
Mtoto 'miaka mitano' amburuza baba polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment