Mkurugenzi wa
idara ya habari maelezo Dokta Hassani Abbas ametolea ufafanuzi suala la
kukatika kwa umeme mara kwa mara jijini Arusha, kwa kuwatoa hofu wananchi
kwamba serikali imeanza kuchukua hatua kwa kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo
pamoja na kufanyia kazi changamoto ya mifumo ya usafirishaji.
Akizungumza
katika kipindi maalumu kilichorushwa na kituo cha utangazaji cha Radio Triple A
leo Dokta Abasi ametaja miongoni mwa changamoto ambazo zinachangia hali hiyo
kwa miaka mingi ni pamoja na kutegemea umeme wa maji pamoja na mabadiliko ya
tabia ya nchi.
Amesema kwa
kuliona hilo serikali imeanzisha mikakati ya kulipatia ufumbuzi kwa kuongeza
vyanzo vya uzalishaji nishati ya umeme ikiwemo miradi mikubwa ya umeme
unaotokana na gesi ya kinyerezi one megawatt 150 ambazo zimeingia kwenye grid
ya taifa
Amesema Kuna
mradi wa upanuzi wa mtambo huo huo wa Kinyerezi one Kinyerezi One Extension
ambao unatarajia kukamilika mwaka huu
ambapo utazalisha umeme mwingine wa megawatt 135.
Pia amesema
Serikali imeanza kujenga mtambo wa Kinyerezi 11 ambao umeshafikia kiwango cha
kukamilika cha asilimia 90 ambapo utaongeza umeme kwenye Grid ya taifa Megawatt
240 na mpaka sasa kuna megawatt 112 zinazalishwa.
Pia
amezungumzia mradi mwingine mkubwa wa kihistoria wa uzalishaji umeme wa
Stieglers Gorge ambao unatarajia kuzalisha umeme wa megawatt 2100 ambao unaenda
kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa nishati ya umeme kwa ajili ya mataifa ya jirani.
Aidha Dokta
Abas ameongeza kuwa serikali imeanza kufanyia kazi changamoto ya mifumo ya
usafirishaji wa nishati ya umeme kwani kukatika kwa umeme kwa sasa kunachangiwa
na mifumo ya umeme na siyo upungufu wa nishati hiyo.
MSEMAJI WA SERIKALI AZUNGUMZIA SUALA LA KUKATIKA KWA UMEME
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment