Wakati idadi
ya wagonjwa wa figo ikiendelea kuongezeka nchini, imeelezwa kuwa Tanzania ina
madaktari bingwa wa figo 13.
Hayo
yameelezwa leo Machi 10, 2018 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile katika hotuba yake mara
baada ya matembezi ya hisani ya umbali wa kilomita 5 kuadhimisha siku ya figo
duniani
"Madaktari
bingwa 13 pekee kwa nchi yetu hawatoshelezi, tupo kwenye mikakati ya
kuhakikisha tunasomesha wataalamu 100 kila mwaka na tunaanza mwaka huu ambapo
wiki ijayo utatoka ufadhili kwa wanafunzi 100," amesema Dk Ndugulile.
Amesema
changamoto ni kubwa kwani nchini wanagundulika wagonjwa wengi wapya wa figo,
hivyo kuna kila sababu ya Serikali kuandaa wataalamu wengi zaidi ili kutoa
matibabu kwa wepesi zaidi.
Rais wa Chama
cha Madaktari wa Figo Tanzania, Dk Onesmo
Kisanga amesema uchache wa madaktari
wa figo nchini upo lakini wanatarajia iwapo Serikali itasomesha wataalamu wengi
zaidi wataweza kuwafikia wananchi waliopo pembezoni
"Tunao
madaktari bingwa 13 nchini kwa sasa lakini wawili wengine watamaliza masomo yao
mapema mwaka huu na wengine watatu watamaliza mwakani hivyo tunatarajia kuwa na
madaktari wapatao 18 ifikapo mwaka 2019," amesema Dk Kisanga.
Mpaka sasa Nchi ya Tanzania ina madaktari bingwa 13 wa figo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 10, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment