Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imepanga Aprili 4, 2018
kusikiliza maombi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSGN), Abdul Nondo
Nondo ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ame[pandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Iringa
Uamuzi huo umetolewa leo Machi 21, 2018 na Jaji
Rehema Samuje wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakama hapo kwa ajili ya
kutajwa.
Hatua hiyo inatokana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za
Binadamu(THRDC), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)
na Mtandao wa Wanafunzi Tanzania(TSNP) kuomba mambo matatu ikiwemo Nondo kupewa
dhamana.
Jaji Sameja ameutaka upande wa Jamhuri kujibu hoja za
utetezi dhidi ya Nondo, Machi 26, 2018
“Kesi ya msingi itakuja kusikilizwa April 4 lakini upande wa
Jamhuri mnatakiwa kuja kujibu hoja za upande wa wawasishaji maombi,” alisema
Jaji Sameja
Nondo asomewa mashtaka mawili, anyimwa dhamana
“Pia upande wa wawasilishaji maombi mnapaswa kuwasilisha
maombi ya nyongeza Machi 27, mwaka huu.”
Machi 19, 2018 THRDC, LHRC na TSNP waliwasilisha
maombi namba 49, 2018 Mahakama Kuu kutaka itoe amri kwa Jeshi la Polisi
kumpeleka mahakamani Nondo.
Wakili wa Nondo, Jebra Kambole amedai maombi hayo
yalifunguliwa dhidi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Mkuu wa
Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo wapeleka maombi
wanaiomba mahakama kutoa amri ya kuletwa mahakamani kwa mwanafunzi Nondo au
kumuachia kwa dhamana kwani ameshikiliwa na polisi kwa muda mrefu bila sababu
za msingi kutolewa.
Hata hivyo, kwa sasa Nondo amenyimwa dhamana na mahakama
mjini Iringa ambayo inataka kujiridhisha na usalama wake
Mahakama Kuu kusikiliza maombi ya Nondo Aprili 4
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 21, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment