Dc aamuru Diwani Kukamatwa

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe John Palingo, ameagiza Jeshi la Polisi kumkamata Diwani wa kata ya Ichenjezya na watendaji watatu wa kata hiyo baada ya kutuhumiwa kufanya ubadhilifu wa fedha za umma Shilingi milioni 17.

Fedha hizo zilitolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo ya kata hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa matundu 28 ya vyoo vya shule ya msingi Ichenjezya.

Aidha mkuu huyo wa wilaya ametoa onyo kali kwa viongozi na watendaji wa serikali kuacha kutumia vibaya fedha za serikali hasa awamu hii ya tano na atakae fanya hivyo hata baki salama.
Wananchi wa Ichenjezya wameshukuru serikali kwa kuchukua hatua hiyo, huku baadhi wakilalamikia watendaji wa kata hiyo kuwa wanawanyanyasa hususani wafanya biashara wadogowadogo na kuomba Rais atembelee wilaya ya Mbozi.


Awali Diwani wa kata hiyo Bahati Mbughi amesema kuwa matumizi yote ya fedha yalishilikisha wananchi kwa kutumia mikutano ya hadhara ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Eric Minga amewataka wananchi kushilikishwa kwenye matumizi ya fedha.
Dc aamuru Diwani Kukamatwa Dc aamuru Diwani Kukamatwa Reviewed by KUSAGANEWS on March 21, 2018 Rating: 5

No comments: