DUNIANI kuna mambo;
wakati kwingineko duniani wafanyakazi mbalimbali huwa wanaandaa migomo na
maandamano kulalamikia mishahara yao midogo wanayopata, nchini Canada ni
kinyume chake.
Madaktari zaidi ya 500
pamoja na wakazi na wanafunzi wa utabibu zaidi ya 150 wametia saini barua ya
wazi wakipinga malipo makubwa wanayolipwa.
“Sisi madaktari wa
Quebec ambao tunaamini katika mfumo imara wa umma, tunapinga ongezko la hivi
karibuni la mishahara iliyoidhinshwa baada ya majadiliano na shirikisho letu la
matibabu,” inasema taarifa hiyo.
Sababu za kupinga
Kundi hili la madaktari
wamesema wamekosewa kwamba watakuwa wanapokea nyongeza wakati manesi na
wagonjwa watakuwa wanahangaika.
“Nyongeza hizi ni za
kushangaza zaidi kwa sababu wauguzi wetu, makarani na wataalamu wengine
wanakabiliwa na hali ngumu sana ya kufanya kazi wakati wagonjwa wetu wanakosa
huduma zinazohitajika kwa sababu ya punguzo kubwa katika miaka ya hivi karibuni
na mamlaka yote kulimbikizwa katika Wizara ya Afya,” inasomeka barua hiyo
iliyochapishwa Februari 25.
“Kitu pekee kwenye mfuko
ambacho kinaonekana kina kinga ya punguzo ni marupurupu yetu,” barua hiyo
inasema.
Canada ina mfumo wa afya
ya umma ambao hutoa matibabu ya jumla ya huduma ya afya za lazima
zinazohitajika kwa misingi ya uhitaji badala ya uwezo wa kulipa.”madaktari 213
wa kawaida na madaktari bingwa 184 na madaktari wakazi 149 na wanafunzi wa
udaktari 162 wanataka pesa zilizotengwa kwa ajili ya nyongeza ya mishahara
irejeshwe kwenye mfuko.
“Tunaamaini kwamba kuna
njia ya kugawa tena rasilimali za mfuko wa afya wa Quebec ili kukuza idadi ya
watu na kukidhi mahitaji ya wagonjwa bila kuwasukuma wafanyakazi hadi
mwisho,” barua hiyo ilisema.
“Sisi madaktari wa
Quebec tunaomba kwamba ongezeko la mishahara lililotolewa kwa
madaktari lifutwe na kwamba rasilimali za mfuko zisambazwe kwa ubora
zaidi kwa manufaa ya wafanyakazi wa huduma za afya zinazostahili watu wa
Quebec.”
Mishahara yao
Daktari nchini Canada
analipwa na Wizara ya Afya Dola za Marekani 211,717 sawa na Dola 339,000 za
Canada kwa huduma za kliniki kwa mwaka kwa mujibu wa ripoti kutoka Taasisi ya
Habari za Afya ya Canada iliyochapishwa Septemba 2017.
Kwa wastani daktari wa
familia analipwa Dola za Marekani 211,717 sawa na Dola za Canada 275,000 kwa
ajili ya huduma za kliniki na mtaalamu wa upasuaji hulipwa Dola za Marekani
354,915 sawa na Dola za Canada 461,000.
Mei, 2016 daktari mmoja
aliweka mchanganuo wa gharama za kuitunza familia yake na ingawa alipokea Dola
Marekani 321,033 sawa na Dola za Canada 300,000 alisaliwa na Dola 136,906 sawa
na Dola za Canada 177,876.
MADAKTARI 500 CANADA WAPINGA ONGEZEKO LA MISHAHARA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment