HOSPITALI YA KENYATA YABATILISHA UAMUZI WAKE WA KUSIMAMISHA KAZI WALIOHUSIKA KWENYE UPASUAJI USIOFAA
HOSPITALI ya Kitaifa ya
Kenyatta (KNH) imebatilisha uamuzi wake wa kuwasimamisha kazi madaktari wawili
walio katika mafunzo na waliohusika katika kisa cha upasuaji wa ubongo wa
mgonjwa asiyehitaji matibabu ya aina hiyo wiki jana.
Hospitali hiyo imechukua
hatua hiyo na kuwasihi madaktari wote waliogoma kurudi kazini.
“Bodi imesimamisha
kabisa hatua za kinidhamu dhidi ya madaktari hao. Tumeachia jukumu hilo bodi ya
chama cha madaktari,” alisema mwenyekiti wa bodi ya KNH Bw Mark Bor wakati wa
mkutano wa wanahabari.
Bodi ya KNH imekutana na
KMPDB pamoja na Waziri wa Afya Bi Sicily Kariuki kujadili suala hilo ambalo
lilifanya madaktari wote walio katika mafunzo kugoma na kuathiri shughuli za
afya hospitalini humo.
Hii ni baada ya daktari
aliyehusika katika kisa cha upasuaji wa ubongo, lakini kwa mgonjwa ambaye
hakuhitaji upasuaji huo, kusimamishwa kazi na KNH.
“Tunawaomba madaktari
kurudi kazini, tunawathamini na kuheshimu kazi yenu,” amesema Bw Bor na
kuongeza kuwa bodi hiyo pia itafanya mkutano na Baraza la Wauguzi ili
kuafikiana kuhusu wauguzi wawili waliosimamishwa kazi.
Kulingana na Waziri wa
Afya Bi Kariuki, kisa hicho kinachunguzwa na shirika la nje na kulitaka kutia
juhudi ili kumaliza uchunguzi huo.
“Ninatarajia bodi ya KNH
itashirikiana na KMPDB kwa kutoa habari inayohitajika katika uchunguzi,”
alisema Bi Kariuki.
Lily Koros
Hata hivyo, Waziri
amekataa kuzungumzia suala la Mkurugenzi Mkuu wa KNH Bi Lily Koros ambaye alimsimamisha
kazi kuhusiana na kisa hicho cha kusikitisha.
Kusimamishwa kazi kwa Bi
Koros kumezua mjadala mkubwa wa kisiasa, suala ambalo mwenyekiti wa KMPDB Prof
George Magoha alisema hangeingilia.
“Kutoka kwa bodi,
tunataka madaktari kurejea kwa sababu hatutaki kuwa na vifo vinavyoweza
kuepukika,” alisema, na kutoa ombi kwa KNH kubatilisha barua dhidi ya daktari
aliyehusika.
“Tumepokea faili zote
zilizo na ripoti kuhusiana na suala hilo, tunataka kurejea kwa madaktari
kurejea kwa nia nzuri, tunataka kufanya haki kwa sababu lazima wahusika
wasikilizwe,” alisema Prof Magoha.
HOSPITALI YA KENYATA YABATILISHA UAMUZI WAKE WA KUSIMAMISHA KAZI WALIOHUSIKA KWENYE UPASUAJI USIOFAA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment