Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguka na kusema watu wanaojifanya kutaka kuandamana wataweza kufanya hivyo kipindi ambacho yeye hatakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam au hakiwa ameondoka ila vinginevyo hawawezi kuthubutu kuandamana.
Makonda amesema hayo
akiwa anahotubia kwenye moja ya mkutano uliofanyika Dar es Salaam na kusema
kuwa watu wengine ambao wanapiga sana kelele kuhusu maandamano hayo na kutaka
kuvuruga amani ya nchi ndiyo wanapata fedha nyingi kutoka wa wafadhili wao
ambao hawataki Mkoa wa Dar es Salaam ubaki salama.
"Kuna kakundi
hapa kanahangaika kweli usiku na mchana wengine wanahangaika kutumia mitandao
ya kijamii kutukana viongozi, kuhamasisha sijui wanaita nini sijui maandamano
nawapa pole sana, watafanya labda mimi nikiondoka nikiwa siyo Mkuu wa Mkoa
kwenye huu Mkoa hiyo mipango mipango yao watafanya labda mimi nikiwa sipo
lakini amani ya mkoa wa Dar es Salaam ni muhimu sana" alisema
Makonda aliendelea
kudai kuwa
"Amani ni muhimu sana kuliko
propaganda za kisiasa na niwaambieni tu wengine wakipiga kelele na kutokea
kwenye 'front page' kwenye magazeti ndiyo wanapata mshahara zaidi, wanapata
donor kutoka kwenye baadhi ya mataifa yasiyotakia amani taifa letu kwa hiyo
lazima tujue tunaye adui tunayeishi naye kama Mtanzania lakini amebeba majukumu
ya mataifa yasiyoitakia amani taifa letu" alisisitiza
Makonda
Maandamano watafanya nikiwa nimeondoka - Makonda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 10, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment