Jumuiya ya Wazazi Arusha Mjini yaja na mkakati yaja wa Kurudisha maadili kwa Vijana

Jumuiya ya wazazi wilaya ya Arusha mjini wanatarajia kufanya kongamanomaalum tarehe 17 mwezi march kwa lengo la kujadili suala la mmomonyoko
wa maadili kwa vijana wa Arusha.

Akizungumza Katibu wa wazazi wilaya ya Arusha Mjini Christopher Pallangyo kwenye mkutano wa kumkaribisha Mwenyekiti wa wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Arusha John Pallangyo amesema kuwa suala la maadili limeporomoka kutokana na jamii kujisahau.

Katibu amesema kuwa wao kama wazazi wana jukumu kubwa la kurudisha
maadili kwa vijana kwasababu yameporomoka kutokana na baadhi ya wazazi kujisahau katika nafasi zao katika familia.

Hata hivyo jumuiya ya wazazi wilaya ya arusha Mjini ina wanachama 8149
kwa mwaka 2017 na walifanya uchaguzi wa kuanzia ngazi ya matawi hadi
taifa ambapo katika wilaya hiyo walifanya uchaguzi kwa asilimia 100.

Kwa upande wa malengo ya jumuiya hiyo Amesema kuwa wamepanga kufanya
ziara kwenye shule zote za msingi na sekondari jijini Arusha ili kutoa
elimu ya maadili kuanzia ngazi ya Chini.

Ameongeza kuwa kwa upande wa mazingira wamepanga kuotesha miti maeneo ya wazi zaidi ya laki 2 kwa kuotesha miti 10000 kila kata kwa kuwa
jiji la Arusha Kuna kata 25 pamoja na kuwapatia wazee kuanzia miaka 60
wasiyo na uwezo vitambulisho vya bima ya Afya CHIF na watawafikia
wazee 250 kwa wilaya nzima ya Arusha Mjini.

Wilaya ya Arusha mjini ni miongoni mwa wilaya saba za mkoa wa Arusha
Tarafa 3 kata 25 ,matawi 61 mashina 783 na mitaa 154 ya chama hicho
cha mapinduzi.
Jumuiya ya Wazazi Arusha Mjini yaja na mkakati yaja wa Kurudisha maadili kwa Vijana Jumuiya ya Wazazi Arusha Mjini yaja na mkakati yaja wa Kurudisha maadili kwa Vijana Reviewed by KUSAGANEWS on March 09, 2018 Rating: 5

No comments: