JPM AWASIHI VIONGOZI WA DINI KUFANYA HILI

Rais John Magufuli amewataka Wahubiri na Maaskofu nchini Tanzania kwa pamoja kuliombea na Taifa na kuwashawishi wananchi wake suala zima la kutambua umuhimu wa kujenga viwanda vya madawa ili kuweza kuzalisha bidhaa zake na kuwapatia vijana ajira.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo leo (Machi 26, 2018) wakati alipokuwa anafanya uzinduzi wa magari mapya 181 ya kusambaza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara eneo la Keko Jijini Dar es Salaam.

"Uchumi wa Viwanda hauwezi kufikiwa bila kuimarisha sekta ya afya, tunatenga bilioni 260 kununua dawa lakini ni 6% tu ndiyo zinanunuliwa ndani. Tengenezeni njia ya kupata wawekezaji watakaojenga viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini, sijui watanzania tumerogwa au shetani amekaa mno hapa, basi tumkemee kwa majina yote akashindwe...
Ili kusudi watanzania tujue ni namna gani tunatakiwa kwa kupata fedha. Niwaombe Maaskofu walihubiri na kulikemea hili na watu wengine wanaojua kuhubiri vizuri tuwaeleza watanzania kwamba tunapoteza bilioni 500 kila mwaka kununua madawa wakati tungekuwa tunatengeneza nchini zingebaki hapa,tunalalamikia mengine yale ya maana ya kuyalalamikia hatuyapigii kelele", amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli ameendelea kwa kusema "kusubiri ni kugumu, tutengeneze njia sasa, Wizara ya Afya kaeni na wafanyabiashara wa ndani muone namna ya kuwawezesha wafungue viwanda vya dawa. Tuwakusanye pia mafamasia wetu tuone namna ya kuwawezesha kufungua viwanda, na majeshi yetu pia. Nasikia mnakwamishana wenyewe hapa, TFDA wanazuia dawa zenu bandarini na wakati mwengine mpaka zina-expire. akizuia tena niambieni halafu nione nani huyo mwenye mamlaka zaidi yangu".

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Mtendaji wa MSD Laurian Bwanakunu amesema baada ya kuongezewa bajeti yao kufikia bilioni 250 kwa sasa MSD wanasambaza dawa zenye thamani ya bilioni 18 na lengo ni kufikia bilioni 21 ikifika mwezi Julai.
JPM AWASIHI VIONGOZI WA DINI KUFANYA HILI JPM AWASIHI VIONGOZI WA DINI KUFANYA HILI Reviewed by KUSAGANEWS on March 26, 2018 Rating: 5

No comments: