Baraza la Maaskofu Wa Katoliki waungana na KKKT kuivaa Serikali

Baraza la Maaskofu Katoliki limeivaa serikali ya Tanzania na kusema kuwa serikali imekuwa ikivunja Katiba na Sheria za nchi kwa kuzuia shughuli za kisiasa kama vile maandamano, mikutano ya hadhara, makongamano, mijadala ambayo ni haki ya kila raia.

Baraza la Maaskofu limetoa ujumbe siku kadhaa zilizopita wakati wakitoa ujumbe wa Kwaresma kwa mwaka 2018 kwa waumini wao na kusema kuwa wao wameamua kuangalia dalili za nyakati zetu Tanzania katika nyanja ya siasa, uchumi na kijamii na kuona ishara ambayo si nzuri.

"Kikatiba, nchi yetu inafuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katiba na Sheria mbalimbali zimeainisha utaratibu wa kazi na shughuli za vyama vya siasa. Ili kuhakikisha kwamba kazi na shughuli za vyama vya siasa zinakuwa endelevu, vyama vyenye kukidhi vigezo hupewa ruzuku kupitia Bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania. Hata hivyo, shughuli za siasa bado zinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola.  Maana yake ni kwamba shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa,  kama vile mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na hata mikutano ya ndani, ambayo ni haki ya kila raia, zimekoma mpaka uchaguzi mwingine. Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na Sheria za nchi"

Aidha Baraza hilo la Maaskofu liligusia kuhusu suala la vyombo vya habari kufungiwa
"Vile vile baadhi ya vyombo vya habari vimefungiwa au kusimamishwa kwa muda, na hivyo kupunguza uwigo wa uhuru wa wananchi wa kupata habari, maoni na wa kujieleza.

 Kufungiwa huku kwa vyombo vya habari kumeenda sambaba na kuminya uhuru wa mahakama na bunge kwa njia ya kuminya haki wabunge na kutowapa nafasi ya mikutano ya hadhara kama haki yao ya msingi ya Kikatiba. Katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu. Kumekuwapo pia hali ya vurugu katika chaguzi mbalimbali.

Chaguzi hizi zinaacha nyuma uchungu, hasira, tama ya kulipa kisasi na hata kususia chaguzi nyingine. Hali hii ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu. Tukiiachia hali hii izoeleke tushishangae huko mbeleni kujikuta katika mifarakano mikubwa zaidi itakayobomoa misingi ya amani na umoja wa kitaifa"

Mbali na hilo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania lilizungumzia sauala la uchumi na kijamii ambapo pia wameonyeshea kidole juu ya mambo mengi maovu ambayo yamekuwa yakitokea hivi karibuni.
Baraza la Maaskofu Wa Katoliki waungana na KKKT kuivaa Serikali Baraza la Maaskofu Wa Katoliki waungana na KKKT kuivaa Serikali Reviewed by KUSAGANEWS on March 26, 2018 Rating: 5

No comments: