Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora
imemhukumu mkazi wa Manispaa ya Tabora, Sadick Masunzu (47) kifungo cha miaka
minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti yake mwenye umri wa
miaka 16 na kumpatia ujauzito
Akitoa hukumu hiyo jana, hakimu wa mahakama
hiyo, Joctan Rushela alisema ameridhika na maelezo yaliyotolewa na upande wa
mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili Tito Mwakalinga kuthibitisha bila shaka
kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo
Hakimu huyo aliongeza kuwa kitendo
kilichofanywa na mshtakiwa si cha kiungwana katika jamii ya Watanzania, hivyo
mahakama inamtia hatiani kwa kosa hilo na inamhukumu kwenda jela miaka minne
ili liwe funzo kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo
Awali wakili wa Serikali, Mwakalinga alidai
mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alimbaka mtoto wake wa kumzaa na kumsababishia
ujauzito
Mwakalinga alidai mshtakiwa alitenda kosa
hilo katika tarehe tofauti Januari 2017 na kumsababishia ujauzito binti huyo
aliyekuwa mwanafunzi wa Sekondari ya Lwanzali iliyopo katika Manispaa ya Tabora
ashindwe kuendelea na masomo
Upande wa mashtaka uliiomba mahakama hiyo
kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kwa kuwa kitendo cha kumbaka na kumtia mimba
mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi kimemharibia maisha yake.
Akizungumza mjini
Dodoma Juni 16, 2017 katika kongamano la maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa
Afrika, aliyekuwa naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk Hamis Kigwangalla alisema mtoto mmoja wa kike kati ya watatu
anakumbana na ukatili wa kingono kabla ya kufikia umri wa miaka 18
“Kwa mujibu wa Takwimu za Elimu kwa Mwaka
2012 hadi 2016 idadi ya watoto wa kike walioacha shule kutokana na kupata
ujauzito ni 610 (mwaka 2011), 2,433 (mwaka 2012), 247 (mwaka 2013), 265 (mwaka
2014 na 251 (mwaka 2015). Serikali inaendelea kukabiliana na changamoto hizi
ili kuhakikisha wanafunzi wa kike wanapata elimu hadi kufikia ngazi ya vyuo,”
alisema Dk Kigwangalla.
Baba afungwa jela kwa kumtia mimba binti yake.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 24, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment