Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amewataka viongozi
nchini kusimamia haki kwa maelezo kuwa Taifa linakoelekea ni kubaya.
Sumaye ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani
amewaomba viongozi wa dini kutokaa kimya na kuwataka kukemea maovu
yanayoendelea kwani ni jukumu lao na si siasa.
Amesema hayo leo Februari 20,2018 katika Kanisa la Mtakatifu
Anna, Hananasif, wakati wa misa ya kumwombea Katibu wa Chadema, Kata ya
Hananasif, Daniel John.
Akitoa salamu za Chadema, Sumaye amesema "Daniel hakufa
kwa kuipigania haki, amekufa kwa kupigania haki. Baba paroko nakuhakikishia hii
si siasa. Chumvi inapokosa radhi hutupwa nje."
"Haki haitendeki, maumivu yanatokea na tunanyamaza,
tunapaswa kutupwa nje na kukanyangwa kanyangwa, Daniel amekuwa chumvi hivyo
ametupwa nje," amesema
Akisisitiza, Sumaye amesema "Katika kupigania haki,
kuna wachache watamwaga damu, Daniel ni miongoni mwao na hao hawatarudi,
hakuna historia hiyo popote damu hiyo itadai itadai."
Sumaye ameongeza "Taifa lote tukemee na wahusika
wakachukua hatua zinazopaswa sina hakika kama zitachukuliwa, pale
tunapozipuuza, tukaona hawachukuliwi hatua, siku damu zitakapodai hakuna wa
kuizuia."
Kuhusu viongozi wa kiroho, Sumaye ameaema "Viongozi wa
dini kemeeni, mnapoona kuna ubaya halafu hamsemi, hii si siasa, kemeeni ni
jukumu letu sote na msipokemea taifa hili linakwenda kubaya."
Amesema Mungu ampokee huko kunakostahili na sisi turejee
katika mstari na kuwa nia njema yenye amani
Sumaye amesema Chama kimesikitika sana kwa yote yaliyotokea
na tangu msiba ulipotokea tumekuwa na familia na tutaendekea kuwa nao mpaka
tutakapomsindikiza katika makazi yake ya milele.
Sumaye amesema Mungu anahusika na uhai wetu lakini sisi
binadamu tunafanya mambo yasiyostahili.
Akitoa salamu za watu waliokuwa wakifanya kazi kwa ukaribu
zaidi ni Severine Kimario amesema zilikuwa taarifa za kushtua kuhusu kifo chake
lakini mwisho wa siku kazi ya Mungu haina makosa
John aliyezaliwa Desemba 26, 1980 , altekwa, kipigwa
na kuuawa na watu wasiojulikana Februari 11,2018 kisha mwili wake kutupwa fukwe
za Coco.
Baada ya misa, mwili wa John unasafarishwa kwenda Mafinga
mkoani Iringa kwa mazishi. John ameacha watoto wawili na mjane mmoja
Baadhi ya viongozi waliohudhuria misa hiyo ni Makamu
Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Profesa Abdallah Safari, Meya wa Ubungo, Boniface
Jacob, mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na mbunge wa Viti Maalum, Susan Lyimo.
Sumaye Taifa linakoelekea ni kubaya.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 20, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment