Mwili wa
aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina
Akwilini unarajiwa kuwasili kesho alfajiri Februari 23, 2018 katika Kijiji cha
Marangu kilichopo Kata ya Marangu Kitowo wilayani Rombo.
Mwili wa
mwanafunzi huyo umeagwa leo Februari 22, 2018 katika viwanja vya chuo hicho na
ndugu kuelekea wilayani Rombo kwa mazishi.
Kwa mujibu wa
ratiba iliyotolewa leo nyumbani kwa baba wa marehemu inaeleza kuwa, baada ya
mwili huo kufika utapelekwa katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya
Olele saa 3:40 asubuhi
Inaeleza kuwa
waombolezaji wataanza kutoa heshima za mwisho saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:00
mchana.
Ratiba hiyo
inaeleza kuwa atakayeongoza ibada ya mazishi nyumbani kwa wazazi wa marehemu
kuanzia saa 7:00 mchana hadi saa 8:30 ni Paroko wa kanisa hilo, Evans
Mavumilio.
Baada ya misa
hiyo, watu mbalimbali watatoa salamu za rambirambi hadi saa 9:00 alasiri ambapo
wataelekea makaburini kwa ajili ya kuuhifadhi mwili wa mwanafunzi
Mwili wa Akwilina Kusafirishwa Rombo kesho asubuhi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 22, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment