MADIWANI WA CHADEMA ARUSHA WAHAMIA CCM


Madiwani 2 kupitia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA katika halmashauri ya jiji la Arusha wamejivua nafasi zao za udiwani na kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha mapinduzi Ccm kwa kile walichodai kuwa ni kumuunga mkono raisi magufuli kwa utendajinkazi wake mzuri wa kazi ya kutumikia wananchi.

Madiwani hao ambao ni diwani wa kata ya Daraja mbili Bwana Prosper Msofe na diwani wa kata ya Terati Bwana Obedi Mosses Meng’oriki wamesema kuwa wameamua kujiunga na chama cha mapinduzi kwa kuwa huko walikokuwa wanaishi kwa migogoro.

Wamesema kuwa chama cha Demokrasia na maendeleo kimekuwa kama chama cha mtu flani ambapo wanakosa uhuru wa kuwatumikia wananchi hivyo wakaona wamuunge mkono raisi kwa kazi anayofanya.

Bwana Msofe amesema kuwa kwa jiji la Arusha chadema kimekuwa chama cha mbunge Godbless Lema jambo ambalo haliwezi kuwaletea wananchi maendeleo huku meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro akikataa kukosolewa kutokana na uwezo wake mdogo wa kuongozahalmashauri hiyo ya jiji la Arusha.

Mpaka sasa kata ambazo madiwani wake wamejiunga na CCM ni kata ya Murieti (Credo Kifukwe) Kata ya Kimandolu(Rayson Ngowi)Kata ya daraja mbili (Prosper Msofe)Kata ya Terati (Obedi Mosses Meng”oriki)

MADIWANI WA CHADEMA ARUSHA WAHAMIA CCM MADIWANI WA CHADEMA ARUSHA  WAHAMIA CCM Reviewed by KUSAGANEWS on February 20, 2018 Rating: 5

No comments: