
Miili ya askari wa Jeshi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) waliouawa na waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC) inarejeshwa nchini leo.
Taarifa ya ofisi ya habari ya JWTZ
imesema miili ya askari hao itawasili nchini leo Jumatatu Desemba 11,2017 saa
kumi na mbili jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA).
Awali, akizungumzia na waandishi wa
habari jana Jumapili Desemba 10, 2017 Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali
James Mwakibolwa alisema miili ya askari hao ingerejeshwa nchini kati ya
Jumanne Desemba 12, au Jumatano Desemba 13,2017 kwa ushirikiano kati ya
Serikali na Umoja wa Mataifa (UN).
Mwakibolwa alisema askari hao
walivamiwa kambini na waasi wa ADF na mapigano yalidumu kwa takriban saa 13.
Alisema askari 14 wa JWTZ waliuawa, 44 wamejeruhiwa na wengine wawili
hawajulikani walipo.
Alisema tukio hilo lililotokea
Desemba 7,2017 katika kambi ndogo iliyopo katika daraja la Mto Simulike,
kaskazini mashariki mwa Wilaya ya Beni, Jimbo la Kivu nchini DRC.
Miili ya askari waliouawa DRC kurejeshwa leo saa 12 za jioni Uwanja wa (JNIA)
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 11, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment