Mbunge wa Mtwara Mjini
(CUF), Maftaha Nachuma amewataka wananchi wa jimbo hilo kupuuza taarifa
zinazosambaa kwamba ana mpango wa kujiondoa katika chama hicho.
Amesema anaendelea
kuwatetea wakazi hao ili wapate maendeleo.
“CUF hawana historia
ya kuhamahama vyama, hata huyo aliyeondoka ameondoka kwa masilahi binafsi. Mimi
Maftaha Nachuma nitakuwa wa mwisho kuondoka CUF,” alisema jana Jumatano Desemba
6,2017.
Alisema suala la
wabunge kujitoa katika nafasi zao linasababishwa na njaa kutokana na kuangalia
masilahi binafsi bila kutetea wananchi.
Nachuma alisema
wabunge wengi walidhani wakipata nyadhifa hizo watakuwa wananufaika kwa kupata
fedha lakini sasa hilo halipo kwa kuwa ubunge siyo dili bali ni kwa ajili ya
kuwatumia wananchi.
Kupitia mitandao ya
kijamii imeelezwa kwamba mbunge huyo ana mpango wa kujiondoa CUF na kujiunga na
CCM.
Nachuma alisema
wanaosambaza taarifa hizo wana nia mbaya ya kumchafua kwa masilahi binafsi.
Mbunge wa Mtwara Mjini (CUF), Maftaha Nachuma Akanusha Kuhamia CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 06, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment