Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani
Madabida na wenzake watano jana Jumatano walipanda kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka sita ya uhujumu uchumi ikiwamo
kusambaza dawa bandia za kufubaza virusi vya Ukimwi ' ARV’s ' na kusababisha
hasara ya Sh 148 milioni.
Kabla ya kusomewa mashtaka ya kesi hiyo mpya ya uhujumu uchumi
namba 80 ya 2017, mahakama ilimfutia kesi iliyokuwa na mashtaka matano
yanayofanana na hiyo iliyofunguliwa mwaka 2014.
Kesi hiyo ilifutwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa
baada ya Wakili wa Serikali, Shedrack Kimaro kuomba iondolewe kwa kuwa
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao.
Kesi hiyo ilikuwa katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa
mashahidi wa upande wa mashtaka na mashadi tisa walikuwa wamekwishatoa ushahidi
wao na washtakiwa walikuwa nje kwa dhamana.
Baada ya kesi hiyo kufutwa, Madabida ambaye ni ofisa mtendaji
mkuu wa kiwanda hicho na wenzake walikamatwa tena na kufunguliwa kesi hiyo mpya
ya uhujumu uchumi.
Mbali na Madabida wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Seif
Shamte ambaye ni mkurugenzi wa uendeshaji, Simon Msoffe (meneja masoko)
na Fatma Shango (mhasibu msaidizi) wa Tanzania Pharmaceutical Industries
Ltd. Pamoja na Sadick Materu na Evans Mwemezi ambao ni maofisa wa Bohari Kuu ya
Dawa.
Baada ya kusomewa mashtaka washtakiwa hao hawakurusiwa kuongea
chochote kwa sababu mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya
kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Wakili wa Serikali, Pius Hilla alisema upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika lakini DPP bado hajafanya maamuzi kama isikilizwe Kisutu ama
Mahakama Kuu.
Washtakiwa hao wanatetewa na Mawakili Denis Msafiri, Makaki
Masatu na Nehemiah Nkoko.
Wakili Msafiri alisema Mahakama ya Kisutu inayo mamlaka ya
kuisikiliza hiyo kwa sababu kiwango chake cha fedha kipo chini ya Sh 1
bilioni ambayo ndiyo inapaswa kusikilizwa Mahakama Kuu.
Kutokana na hoja hiyo Wakili Hilla aliomba wapewe muda hadi
leo Alhamisi ndiyo wajibu hoja ya upande wa utetezi.
Hakimu Nongwa aliiahirisha kesi hiyo hadi leo Alhamisi
kutokana na ombi hilo na kuamuru washtakiwa wapelekwe polisi hadi leo
Alhamisi itakaposikilizwa hoja kama mahakama hiyo ina mamlaka ya kuisikiliza
kesi hiyo ama la.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM sasa Ashitakiwa kwa Uhujumu Uchumi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 06, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment