Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameagiza
utekelezaji wa Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira uwe ni ajenda ya kudumu
ya kila ngazi ya Uongozi.
Makamu wa Rais
ameyasema hayol eo wakati wa Uzinduzi wa Kamapeni ya Taifa ya Usafi wa
Mazingira awamu ya Pili ukiofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi
Chang’ombe,mkoani Dodoma.
Makamu wa Rais alisema
Serikali imejiwekea mikakati mbali mbali ya kupambana na maradhi ya kuambukiza
ambapo usafi wa mazingira ni njia mojawapo ambapo katika awamu ya kwanza ya
kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira ambapo jumla ya kaya 1,662,550
zilijengwa vyoo na shule 2,133 vilijengwa vyoo bora.
Katika awamu ya Pili
iliyozinduliwa leo kaya 5,600,000 zinatarajiwa kuongeza idadi ya vyoo
bora na shule za msingi 3,500 na sekondari 700 zitapata huduma ya vyoo bora na
sehemu maalum ya kunawa mikono baada ya kutoka chooni.
“Wahenga
walisema Samaki mkunje angali mbichi, methali hii inatukumbusha jukumu la
kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa usafi wa mazingira tangia wadogo wakiwa
mashuleni”alisisitiza Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais alitoa
Wito kwa Wanawake wote nchini kujifunga Kibwebwe na kujenga vyoo, alisema
Wanawake wamekuwa na vikundi mbali mbali vya kusaidiana na kuwezeshana hivyo
kwa kupitia vikundi hivyo wanaweza kufanikisha ujenzi wa vyoo bora majumbani.
Makamu wa Rais
aliwapongeza Washindi wote wa Afya na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2016/17. Pia
aliwashukuru wadau mbali mbali ambao wamechangia kwa namna moja au
nyingine kufanikisha uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya Taifa ya
Usafi wa Mazingira.
Makamu wa Rais azindua rasmi kampeni ya Kitaifa ya usafi awamu ya pili,Dodoma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
December 08, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment