Spika mstaafu wa Bunge, Anne Makinda amesema wakati wa wanawake kusubiri kuwezeshwa umepita.
Akiwasilisha mada kwenye tamasha la jinsia linaloendea kwenye viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Makinda amesema bidii, weledi na kupanga muda wake ipasavyo ndivyo vilivyomfikisha alipo.
"Wanawake acheni kujidekeza, wakati wa kudhani kuna mtu wa kuja kuwainua umepita. Simama na onyesha kwamba unaweza," amesema.
Amewataka wanawake kujifunza kusema kidogo na kusikiliza zaidi, pia kufanya jambo ili watu wajue aliyefanya ni nani.
Makinda amewataka wanawake kuwa jasiri na kutokubali kujiingiza kwenye mapenzi kwa kurubuniwa kupewa kile wanachotaka ikiwemo vyeo vya kisiasa.
"Acheni mapenzi kwenye shughuli za kazi, siri ya mafanikio ni nidhamu na kujiamini. Siku zote unakuwa unaweza," amesema.
No comments:
Post a Comment