Samia Awapa makavu wanawake

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake kote nchini kutumia fursa za kiuchumi wanazozipata ili kupunguza umasikini uliokithiri haswa kwa wanawake waishio vijijini.

Mhe.  Samia amebainisha hayo jana katika uzinduzi wa tamasha la 14 la jinsia lililoandaliwa na mtandao wa wanawake nchini TGNP ambapo amesema kuwawezesha ni nyenzo muhimu katika kukuza usawa wa kijinsia pamoja na kufikia uchumi wa kati.

Aidha makamu wa rais amemuagiza kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kuhakikisha madawati ya kijinsia yanafanya kazi ipasavyo ili kumaliza kushughulikia changamoto za wanawake ikiwemo ukatili.

Pamoja na hayo Mh. Samia amewataka wanawake kuheshimu familia pamoja na nafasi walizo nazo ili kujenga familia zilizo bora. "Mimi nikirudi nyumbani huwa napiga goti kwa mume wangu ili kuboresha mahusiano mazuri pamoja na kujenga familia bora.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TGNP Dkt. Vicensia Shule amesema bado suala la unyanyasaji linatakiwa kufanyiwa ufumbuzi na kuwa asilimia 32 ya wanawake wanaishi katika umasikini.

Samia Awapa makavu wanawake Samia Awapa makavu wanawake Reviewed by KUSAGANEWS on September 06, 2017 Rating: 5

No comments: