Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Bw. Kailima Kombwey ametangaza kumteua Mbunge ndugu Rehema Juma
Migira kuwa Mbunge wa viti maalum kupitia Chama Cha (CUF) kufuatia kifo cha
mbunge mteule Bi Hindu Mwenda aliyefariki dunia Septemba 1, 2017.
Kailima
amesema Tume ya Uchaguzi imefanya uteuzi huo baada ya kupata taarifa kutoka wa
spika wa bunge, Job Ndugai kuwepo kwa nafasi moja ya ubunge kufutia kifo cha
mbunge huyo mteule ambaye alifariki siku tatu kabla ya kuapishwa.
"Tume ya taifa ya uchaguzi imemteua
ndugu Rehema Juma Migira kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada
ya kupata taarifa kutoka wa spika ambaye alitutaarifu kuwepo kwa nafasi moja ya
wazi ya viti maalumu kupitia chama cha CUF baada ya aliyeteuliwa kuwa mbunge wa
viti maalum CUF kufariki dunia" alisema Kailima
Aidha
Kailima aliendelea kusema kuwa tume hiyo imefanya uteuzi pia wa madiwani wa
viti maalum watatu kujaza nafasi wazi katika halimashauri za Tanzania bara
madiwani hao ni pamoja na ndugu Jane Chungwa kutoka CCM ambaye anakuwa diwani
wa viti maalum halmshauri ya Itigi Singida, Ndugu Osana Mwinyi kutoka chama cha
CCM anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Bahi Dodoma na ndugu Pili
Mfaume kutoka chama cha CUF anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Temeke,
uteuzi huo wa madiwani umefanyika baada ya tume kupata taarifa ya kuwepo kwa
nafasi hizo wazi kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa.
No comments:
Post a Comment