Aliyetajwa fisadi Magufuli amkingia kifua



Rais Dkt. John Magufuli amemkingia kifua aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Makinikia Prof.  Abdulkarim  Muruma na kusema kuwa ndiye mtu aliyekuwa akifanya kazi ya uchunguzi na kutoa taarifa taari za ufisadi migodini na kusema za migodini.

Akizungumza leo wakati akipokea taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai ambapo katika taarifa  ya ripoti iliyotolewa jana ilimtaja Prof Mruma na kudai kuwa ni mtu aliyeisababishia nchi hasara kupitia Almasi na Tanzanite akiwa Mwenyekiti Kamati ya Ukaguzi Madini.

Rais Mgufuli amesema kuwa uchunguzi  wa uwizi uliokuwa ukifanya kwenye madini ulianza muda mrefu lakini wakati alipokuwa anazungumza kuhusu masuala haya ya wizi wapo watu wengine waliomuona anazungumza kutoka hewani

"Tumekuwa tukiwatumia baadhi ya watanzania ambao ni wazalendo ku-risk maisha yao ili tupate taarifa kuhusu Tanzanite. Najua mna flash japo hamjanikabidhi, lakini mimi pia ninayo ya kwangu nmekaa nayo muda mrefu sana. Nataka niwaambie wapo wazalendo wanaofanya kazi kule. Hii ni Vita na maaskari wanapokuwa vitani hutoa watu kwenda kuwa maadui ili kupata taarifa mtashangaa aliyetupa taarifa zote hizi ni Profesa Mruma na ni yeye ametuwezesha kujua ni wapi tunaibiwa na kwa kiasi gani" Magufuli.

Rais ameongeza kuwa  "Aliyevumbua mabaya, mwenye kutoa taarifa zote ni Mruma. Hadithi ya kumtuma askari vitani upande wa maadui ndiyo inakuja hapa. Hivyo niwahakikishie wapo watu wetu ambao wanafanya kazi huko za kizalendo kwa ajili ya maslahi ya taifa na kwa kuwa wanajichanganya nao hawawezi kuwafahamu.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa anazo data za kutosha kuhusiana na ufisadi unaoendelea migodini  kwani  taarifa zote ikiwa ni pamoja na mipango ya kuibia taifa na hata watu hao waliposhtuka walibadilisha computer zao na ikawa tayari wameshachelewa kwani wao walikuwa na taarifa zote mapema kabla ya mabadiliko hayo. 
Aliyetajwa fisadi Magufuli amkingia kifua Aliyetajwa fisadi Magufuli amkingia kifua Reviewed by KUSAGANEWS on September 07, 2017 Rating: 5

No comments: