Polisi Mkoani Geita wanamshikilia kijana Samson Petro (18) mkazi wa Katoro wilayani Geita mkoani hapa Kwa tuhuma za kuteka watoto katika mikoa ya Arusha na Geita
Kijana huyo amekamatwa usiku wa Septemba 2 ,saa mbili usiku katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungulu iliyopo mji mdogo wa Katoro
Kamanda wa polisi mkoani humo ,Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kukamatwa Kwa kijana huyo na kusema polisi linaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani
Hivi karibuni jeshi la polisi mkoani Arusha lilitoa taarifa za kijana ajulikanae kwa Jina la Samsoni Petro ambaye alitoroka baada polisi kuguundua kuwa ndiye mhusika wa matukio ya utekaji Arusha ambapo watoto wawili Morin na Ikram Bado hawajapatikana.
No comments:
Post a Comment