Nitawafutia uraia

 Waziri wa mambo ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba ametishia kuwafutia uraia watanzania wapya wa Katumba mkoani Katavi ambao walikuwa wakimbizi kwa muda mrefu kutokana na tabia ya ya baadhi yakubaguana kitaifa na kikanda.Waziri Nchemba amesema hayo leo wakati  alipopita kwenye kambi kuangalia usajili unaendeleaje ambapo amesema  wananchi   hao waliopewa uraia wakitokea burundi wakati wa vita ya kikabila miaka 1972 wamekuwa na tabia ya ubaguzi hata kufikia kushindwa kusaidiana kwenye biashara zao.

Waziri amewaambia wananchi hao kuwa yeyote atakayeleta mambo ya ubaguzi ikiwa ni pamoja na kubaguana kibiashara  katika jamii hatosita kumfutia uraia alioupata kwani Watanzania hawana mambo ya kibaguzi.

Pamoja na hayo Kiongozi huyo ametumia muda huo kuwataka Watanzania kuwa na utanzania ndani ya mioyo yao na waache tabia ya kutaka kukwamisha kila kitu kinachofanywa na serikali kwa kuweka vikwazo mbele ili vitu visifanikiwe.

Nitawafutia uraia Nitawafutia uraia Reviewed by KUSAGANEWS on August 22, 2017 Rating: 5

No comments: