Mahakama Kuu nchini Uganda, imemhukumu kifungo cha maisha jela kiongozi wa kundi la Kiislamu la Tabliq Sheikh Mohammad Yunus Kamoga kwa makosa ya ugaidi.
Mbali na Sheikh Kamoga, wengine waliopewa adhabu hiyo kali ni pamoja na Sheikh Siraje Kawooya, Sheikh Murta Mudde Bukenya na Sheikh Fahad Kalungi.
Licha ya kupatikana na kosa hilo, Mahakama imewafutia makosa ya kuwauwa viongozi wengine wa Kiislamu Sheikh Mustafa Bahiga, Ibrahim Hassan Kiryana miongoni mwa wengine.
Mahakama hiyo ikiongozwa na Jaji Ezekiel Muhanguzi, imeamua pia Kakande Yusufu maarufu kama Abdallah na Sekayaja Abdulsalam maarufu kama Kassim Mulumba wahukumiwe jela miaka 30 kwa makosa hayo ya ugaidi lakini ikaeleza kuwa kifungo chao ni tofauti kwa sababu, wao walikuwa ni wafuasi tu.
Hata hivyo, wakili wao Fred Muwema amesema kuwa, atakataa rufani kupinga hukumu hiyo ambapo Mahakama imesema, wafungwa hao wana siku 14 kufanya hivyo.

No comments:
Post a Comment