Polisi waendelea kumganda Tundu Lissu

Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amekwama kupata dhamana leo tena hivyo atalala rumande kwa siku ya pili Police Central.Afisa Habari wa CHADEMA Tumaini Makene amefunguka na kusema kuwa Mwanasheria huyo amekwama kupata dhamana leo na kudai wanasubiri kesho ili kuona kama itawezekana kupata dhamana akiwa mikononi mwa polisi au mahakamani. 

"Jitihada za kuhakikisha Lissu anapata haki yake ya kisheria ya kupata dhamana leo zimeshindikana. Hivyo bado yuko polisi tunasubiri utaratibu mwingine kesho wa ama kupata dhamana akiwa mikononi mwa polisi au kufikishwa mahakamani" alisema Tumaini Makene 

Mapema leo jeshi la polisi liliongozana na Mwanasheria huyo mpaka nyumbani kwake Tegeta na kwenda kufanya upekuzi kufuata makosa mawili anayoshikiliwa nayo likiwepo kosa la kusema hadharani makosa ya Rais na kosa la pili ni uchochezi kufuatia taarifa alizozitoa kuhusiana na kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Canada. 

Polisi waendelea kumganda Tundu Lissu Polisi waendelea kumganda Tundu Lissu


Reviewed by KUSAGANEWS on August 23, 2017 Rating: 5

No comments: