Na Ibrahim Yassin,Rungwe
SIKU chache baada ya Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Rungwe mkoani Mbeya,kumkamata na kumhoji kwa saa kadhaa afisa mtendaji wa kata ya Lufingo Rehema Maraso, kwa tuhuma za kutoza faini pasipo kutoa lisiti,hatimaye mwenyekiti wa kijiji cha Simike na wenyeviti wa vitongoji vyote nane wamejiuzuru nyadhifa zao wakidai hawako tayari kufanya kazi na Mtendaji huyo.
Wakizungumza jana na gazeti hili,wenyeviti hao walisema afisa huyo amekuwa akiyatumia vibaya madaraka yake ikiwemo kutosoma mapato na matumizi ya fedha za maendeleo zitokanazo na michango ya wananchi na kibaya zaidi aliwapeleka mahakamani kwa kosa lisilofahamika.
Akizungumzia hali hiyo,mwenyekiti wa kijiji cha Simike Eprahim Kapondania,alisema awali walikaa na kujadili namna ya kujenga zahanati ya kijiji ambapo tulikubaliana kila kitongoji kihakikishe kinakusanya Tsh,Milioni 1.5 na kuzikakabidhi kwa afisa huyo ambapo ambaye hakuwahi kuwasomea mapato.
Abraham Mwasinyanga Mwenyekiti wa kitongoji cha Kalalo,(CCM) alisema baada ya kuchangasha fedha hizo walizopewa lengo,ni kijiji kitongoji kimoja tu cha Ibabu kilichofikia lengo la Mioni 1.5 lakini vitongoji vyote fedha zilifeli kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa na kipato ambapo baadhi ya vitongoji zilifeli fedha laki 2 hadi 5.
Alisema kutokana na kufeli kwa fedha hizo afisa huyo aliamua kuwashitaki na kuwapeleka mahakamani na kuwafungulia shitaka la kutofikia lengo la makusanyo lakini mahakama ya mwanzo kata ya Kiwira iliwaachia huru na kueleza suala lirudi kwenye serikali ya kata ili kujadiliana na kuondoa tofauti.
Stephen Kapange, Mwenyekiti kitongoji cha,Ntetesyele ( Chadema) alisema mbali na sakata hilo la kupelekwa mahakamani kwa kutofikia lengo kuna tuhuma nyingine inayomhusu mtendaji huyo,ya kukusanya Tsh,2,20,000/ kila kitongoji kwa ajili ya ujenzi wa maabala lakini ni zaidi ya miaka miwili sasa hakuna kinachoendele.
Alisema yeye na wenzake pasipo kujali itikadi za vyama vyao vya siasa,wameamua kushirikiana kuachia madaraka ili kuondoa lawama kwa wananchi kwa kuwa wao ndiyo wanaolaumiwa wakati aliyeharibu ni afisa mtendaji wa kata na kuwa tayari wameandika barua kuzipeleka kwenye vyama vyao.
Akizungumzia kujiuzuru kwa wenyeviti hao,Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Ezekiel Mwakota,licha ya kukiri kuwepo kwa hali hiyo,alisema halmashauri yake haijapata barua rasmi na kwamba ili kujiridhisha na hilo,wameitaarifu kamati ya siasa ya ccm wilaya kwenda kijijini humo kuzungumza na wenyeviti hao.
Mwakota ambaye pia ni diwani wa kata hiyo hiyo ya Lufingo kupitia (CCM) walikojiuzuru wenyeviti hao,alisema wanasubiri kupata taarifa kutoka kwenye Chama ili kujua ni namna gani watakavyoliweka sawa jambo hilo.
Katibu tawala wilayani humo,Moses Mashaka amekiri kuwepo na hali na kusema kuwa bado ofisi ya mkuu wa wilaya haijapata barua endapo barua itafika kuhusu wenyeviti hao kuachia ngazi taratibu za kuwapata wenyeviti wepya zitafanyika.
Wenyeviti waliojiuzuru na vitongoji vyao,1- Abraham Mwasinyanga (kalola) ccm ) 2-Bonifas Mbange (Kakuyu) ccm) 3- Gwakisa Seme (Itebe) ccm) 4- Monica Nzobe (Ibabu) ccm) 5- Stephen Kapange ( Ntetesyele) Chadema) 6- Nsubiri Mwaisania (Malibila) Chadema) 7- Eliza Mwakapila (Ipyana) ccm) 8-Masebo Bonifas ( Kasanga) ccm) na Ephrahim Kapondania mwenyekiti wa kijiji cha Simike.
Ally Mwakalindile,mwenyekiti wa CCM wilayani humo,alisema hajapata taarifa kuhusu wenyeviti wake kujiuzuru na kwamba anafanya mawasiliano na katibu ili kujua,huku mwenyekiti wa Chadema wilayani humo,Seif Suleiman alisema wenyeviti wake wapo sahihi kujiuzuru kutokana na utendaji usioridhisha wa Mtendaji huyo.
Hata wananchi kwa upande wao,walitaja kusikitishwa na kitendo cha afisa mtendaji huyo,alisimamia kamati ya siasa ya ccm kata kumvua uanachama mwenyekiti wa kijiji cha kalalo ambacho hadi leo hakina mwenyekiti huku shughuri za wananchi zikisuasua.

No comments:
Post a Comment