Niondoke mimi au uondoke wewe

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani ametishia kuwatumbua vigogo wa shirika Umeme Tanzania (TANESCO) akiwemo Mkurugenzi Mtendaji ikiwa watashindwa kutekeleza maagizo matatu likiwemo la kuwaunganishia umeme wakazi 350 wa Kigamboni. Dk Kalemani amesema hayo leo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa vituo vya kupoozea umeme vya Kurasini na Kigamboni.

“Kama maagizo haya hayatafuatwa ama niondoke mimi au uondoke wewe na watendaji wengine, kama mtashindwa kutekeleza mnieleze hapa hapa,” amesema.

Awali Dkt Kalemani alisema kuna wakazi 350 wa Kigamboni ambao walishailipia TANESCO ili waunganishiwe umeme lakini wamekaa muda mrefu bila kupata huduma hiyo ambapo amtaka atekeleze maagizo hayo yakamilike itakapofika Agosti 30 kabla hajachukua hatua zingine. 

“Tafuteni vifaa kama nguzo za umeme popote zilipo lakini nataka wafungiwe kama nilivyoagiza kwa kuwa nimechoka na malalamiko yao,”alisema.

Niondoke mimi au uondoke wewe Niondoke mimi au uondoke wewe Reviewed by KUSAGANEWS on August 22, 2017 Rating: 5

No comments: