Hii ni chuki, hofu, uwoga au ni nini?

Mbunge wa Tarime Vijijini kwa tiketi ya CHADEMA, John Heche amefunguka na kusema serikali haipaswi kuogopwa bali inapaswa kuheshimiwa pale inapopaswa kuheshimiwa na kusema vitendo vya kuwakamata wapinzani ni kutaka kuwatisha na kuwafanya wawe na hofuMbunge Heche amesema hayo leo baada ya jeshi la polisi kumkamata Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu wakati akitoka mahakamani kusikiliza kesi ya uchochezi na kupelekwa Central Police.

" Kwanini serikali hii inayojitapata kuwa ya waadilifu haitaki kuhojiwa kwanini inataka kutishia watu waiogope? Serikali haipaswi kuogopwa inapaswa kuheshimiwa pale inapostahili heshima, kwanini wanalazimisha vitisho na kujaza watu hofu!? Sisi hatutaogopa Aluta continua kamanda Lissu" alisisitiza Heche 

Julai 20 mwaka huu Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA alikamatwa na jeshi la polisi Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) akielekea Kigali, nchini Rwanda na baadaye kufunguliwa mashtaka ya uchochezi.  

Hii ni chuki, hofu, uwoga au ni nini? Hii ni chuki, hofu, uwoga au ni nini? Reviewed by KUSAGANEWS on August 22, 2017 Rating: 5

No comments: